MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 26 November 2014

TAARIFA KAMILI ILIYOTIKISA YA HOUSE GIRL KUNYANYASA MTOTO IMEFIKIA HATUA HII

Msichana huyu wa kazi anaitwa Tumuhairwe ana umri wa miaka 22 na sio 25 kama ilivyoripotiwa ambapo ana siku 26 tu toka aanze kufanya kazi kwenye familia ya mtoto huyo.



Kwa sasa yuko rumande kwenye gereza la Luzira Uganda na atafunguliwa mada ya kutaka kuua.

–  Unaambiwa haya yote yasingejulikana kama Polisi isingemkamata baba mzazi wa mtoto huyu, yani baba alipoona ile video ndio akampiga Msichana huyu wa kazi ambae baada ya kipigo alikwenda kumshitaki baba wa mtoto Polisi.

Polisi walipomchukua Erick Kamanzi (Baba wa mtoto) nyumbani kwa ke na kumfikisha Polisi ambako alieleza sababu za kumpiga Msichana huyu na kuwaonyesha Polisi hii video hapa chini ambayo ni ya tukio la mtoto wake kupigwa.

Baada ya hapo Polisi ndio wakamwachia na kumkamata Msichana huyu wa kazi.
Erick ambae ndio baba mzazi wa mtoto huyu amesema wanashukuru Mungu mtoto kuwa hai bila matatizo na sasa mtoto amekua karibu na baba yake zaidi.



Tarehe 8 December ndio atapandishwa Mahakamani kusomewa mashitaka yake.
November 24 2014 Waziri wa mambo ya vijana wa Uganda aliitembelea familia ya mtoto huyu baada ya watu kuanza kusambaza habari kwamba mtoto huyu alifariki, taarifa ambazo sio za kweli.

Na Mwanaharakati.

No comments: