Na Saidi Mkabakuli,
Mbaba Bay
Timu wakaguzi wa
miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango imetembelea Bandari ya
kimkakati ya Mbaba Bay iliyopo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kujionea shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Bandari hiyo.
Akizungumza wakati
wa ziara hiyo, kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alisema kwamba Bandari hiyo ni
muhimu kwa uchumi wa nchi kwa kuzingatia eneo la kijiografia la bandari hiyo.
“Bandari hii ni
muhimu kwani kijiografia inaweza kuzifikia nchini nyingi zilizo kusini mwa nchi
yetu hivyo inaweza kutumika kama lango la kibiashara miongoni mwa jirani zetu
licha ya uhaba wa miundombinu yake,” alisema.
Aliwasihi
wafanyakazi wanaoihudumia Bandari hiyo kufanya kazi kwa bidii bila ya kuchoka
ili kuweza kuvutia wafanyabiashara na watumiaji wengine kuendelea kuitumia
bandari hiyo.
Kwa upande wake,
afisa bandari ya Mbaba Bay, Bw. Jarome Urio aliutaarifu ugeni huo kuwa Mamlaka
ya Bandari ipo katika mkakati wa kuindeleza bandari hiyo ili kuweza kuihudumia
wateja wengi zaidi.
Pia, Bw. Urio
aliwashukuru wajumbe wa timu hiyo ya ukaguzi kwa kwenda kuitembelea na kujionea
maendeleo ya bandari hiyo.
“Tunafarijika sana
kuona viongozi wa serikali wanapokuja kututembelea kwani hali hii uongeza
hamasa ya utendaji kazi wetu,” alisema.
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012
– 2015/2016) bandari ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye
lengo la kufungulia fursa za
ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi wa uchumi kwa watu walio wengi.
Vipaumbele vingine ni Kilimo ambapo
lengo kuu likiwa ni kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo ili
kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya kuuza nje ya nchi; Maendeleo ya
viwanda: Msisitizo umewekwa katika kuvutia, kuanzishwa na kuendeleza viwanda
vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini (kama vile viwanda vya nguo,
mbolea, saruji, makaa ya mawe, chuma na bidhaa za chuma) na pia sekta ya madini
kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment