Mahakama ya hakimu mkazi Bukoba, imeamua kuwa vikao vya baraza la madiwani viendelee kwani kesi inakwamisha maendeleo ya wananchi wa manispaa ya Bukoba. | ||||||||
Mh Maweda akiwa ofisini |
Hakimu Samweli Maweda, amewaeleza mawakili wa mlalamikaji Anatory Amani, na mlalamikiwa mkurugenzi manispaa ya Bukoba kuwa, ofisi za manispaa ziendelee na kazi zake kama kawaida ambapo shauri la Bwana Aman litasikilizwa tarehe 19 januari 2015, akama mawakili walivyoiomba mahakama, japo mahakama ilikuwa tayari kusikiliza kesi hiyo mpaka mwisho bila kuhalishwa.
Amesema kuwa ubishi wa mlalamikaji hauwezi kuwanyima haki wananchi ya kufanyiwa masuala ya maendeleo kwa kupanga bajeti na kupitisha masuala ya miradi ya maendeleo ya manispaa yao, hivyo yeye kama hakimu ameamua baraza liendelee kujadili masuala yake chini kaimu meya bwana Alexander Ngalinda.
Kwa upande wake wakili wa serikali anayemtetea mkurugenzi wa manispaa, awali alitoa udhulu mahakamani kuwa kesi hiyo isikilizwe haraka, au ihalishwe hadi mapema mwaka kesho, kwasababu yeye ana majukumu mengine yanayomuitaji uwepo wake kule Morgoro, Arusha na Da es salaam, kati ya tarehe 14 nov, na 19 2014.
Baadhi ya sababu alizozitaja mahakamani, wakili huyo mh,. Ngatare, amesema kuwa ni pamoja na marekebisho ya sheria za fedha, masuala ya uchaguzi serikali za mitaa, pamoja na kupeleka taarifa za kuvuliwa udiwani kwa madiwani sita wa manispaa ya Bukoba waliovuliwa na mahakama, ili waziri apitie kutoa maamuzi kama anabariki wasalie bila udiwani au lah.
Wakili Kabunga kushoto akiwa na Mh Alexander Ngalinda kulia |
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment