Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), imeandaa mdahalo huo maalumu wa Katiba kwenye Ukumbi wa Mlimani City ambao mzungumzaji mkuu ni Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Joseph
Butiku amesema kwamba mdahalo huu wa amani ni kwa ajili ya Watanzania wenye
mapenzi mema na ukowazi, ikiwa ni sehemu ya kuziba pengo la mdahalo wa Katiba
uliovunjika Novemba 2 ambao ulifanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl.
Ulivunjika baada ya kutokea vurugu
zinazodaiwa kuanzishwa na kikundi cha watu kwa lengo la kuvuruga uwasilishwaji
wa ujumbe wa Katiba, huku Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM, Paul Makonda
akitajwa kinara wa vurugu hizo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment