Jana kwenye mitandao mbalimbali ya
kijamii kulikuwa na taarifa zinazodai kuwa Lilian siyo raia wa Tanzania na
kwamba anatokea Rwanda.
Akizungumzia tuhuma hizo, Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa mashindano ya Miss
Tanzania, Hashim ‘Uncle’ Lundenga alisema tuhuma hizo kuhusu Lilian siyo kweli.
“Sisi
tunajua Lilian ni Mtanzania, tunaangalia cheti cha kuzaliwa alichotuletea
kamati yetu ambacho kinaonyesha alizaliwa Tanzania, pia ni Mtanzania, hayo
yanayosemwa kwamba Lilian siyo Mtanzania hatuyajui kabisa,” alisema Lundenga.
Pia Lundenga alisema kitendo cha
Sitti Mtemvu kujivua taji la Miss Tanzania 2014 kumemnyima sifa ya kuendelea
kushikilia taji la Miss Temeke na lile la Kitongoji cha Chang’ombe.
“Sitti
amevua taji la Miss Tanzania maana yake ni kwamba hata lile la Miss Temeke 2014
na lile la Miss Chang’ombe 2014 ambayo ndiyo alikuwa mshindi kabla ya kushinda
lile la taifa, ameyavua pia,” alisema
Lundenga.
Sitti aliingia katika kashfa ya
tuhuma za kudanganya umri baada ya nyaraka zake mbalimbali kuonyesha amezaliwa
1989 na siyo 1991 kama alivyowasilisha kwenye kamati ya Miss Tanzania.
Kwa mujibu wa sheria za mashindano
hayo, mshiriki anatakiwa awe na umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi
miaka 24.
Mwandaaji wa mashindano wa Miss
Temeke, Ben Kisaka alisema, “Waliotoa
taarifa ya Sitti kujivua taji ni kamati ya Miss Tanzania, hivyo wao ndiyo
wanapaswa kutoa taarifa zingine kuhusu taji la Temeke.”
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment