Wapiganaji wa Islamic State katika
jimbo la Anbar,Syria Marchi 2014
Wapiganaji wa kundi la Islamic State
wafungua kambi za mafunzo LibyaWapiganaji wa kundi la Islamic State wameanzisha
kambi za mafunzo mashariki mwa Libya, amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya
masuala ya Afrika.
Libya imekuwa katika mgogoro tangu
kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, ambapo makabila
mbalimbali, wanamgambo na makundi ya kisiasa, wote wakipigania madaraka.
Makundi mbalimbali ya Kiislam
yanawania madaraka mashariki mwa Libya, hukubaadhi yakitangaza kuwa na
ushirikiano la kundi la Islamic State, IS.
Wapiganaji kutoka kikundi cha IS
wakipakia mabaki ya kile kinachosemekana kuwa mabaki ya ndege ya Marekani
isiyotumia abiria baada ya kukonga katika mnara wa mawasiliano huko Raqqa
Septemba 23,2014Akizungumza mjini Washington Jumatano, Jenerali Rodriguez bado
haijafahamika ukaribu uliopo kati ya watu wanaopata mafunzo hayo na kundi la
IS.
"Kikubwa ni watu wanaokuja kupata
mafunzo na msaada wa vifaa kwa ajili ya kambi za mafunzo kwa sasa,"
amesema. "kwa sasa mafunzo hayo bado ni ya hatua ya chini sana na
tunafuatilia kuona namna hali inavyokwenda."
Watoto wakikimbia kando ya mlima
hukumoshi ukisambaa angani kufuatia mapigano katika eneo hilo la mji wa Kobani,
wakati majeshi yanayoongozwa na Marekani kushambulia wapiganaji wa Islamic
StateWaandishi wa habari wanasema katika kipindi cha mapinduzi yaliyomwondoa
madarakani Gaddafi, wapiganaji wengi waasi waliondoka nchini humo kwenda
kujiunga na vikundi vya wapiganaji nchini Syria na baadhi yao wanaaminika kuwa
wamerejea nyumbani(Libya).
Serikali iliyochaguliwa imepoteza
miji mikuu mitatu ya Libya huku kukiwa na mgogoro wa kisiasa.
Benghazi, mji wa pili kwa ukubwa nchini
Libya, uko mikononi mwa wapiganaji wa Kiislam, na bunge linalotambuliwa
kimataifa kwa sasa linaendesha vikao vyake katika mji ulioko pwani ya Tobruk
mashariki mwa nchi hiyo
Marekani imekuwa ikiongoza washirika
wa kimataifa kufanya mashambulio ya anga dhidi ya IS nchini Iraq na Syria
katika miezi ya karibuni.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment