MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 4 December 2014

BALOZI KAMALA;UMOJA WA ULAYA SASA KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI NCHINI NA AFRIKA MASHARIKI

Nchi mwanachama wa jumuiya ya afrika mashariki zitaanza kutekeleza makubaliano yaliyosainiwa kwenye  mkataba wa uchumi na biashara yaani Economic Patnership Agreement EPA, kati yake na nchi za jumuhiya ya Ulaya EU. Mwenyekiti wa mabalozi wa jumuhiya ya afrika mashariki ambaye pia ni balozi wa Tanzania nchini Ubelgij Mh Deodorous Kamala, amesema kuwa mazungumzo ya kukamilisha mkataba huo yalianza mwaka 2002, na yamekamilika November 14/2014 . 

Mambo muhimu katika mkataba huo ni pamoja na uhusiano huo wa kikanda usifungwe na makubaliano yao kati ya ACP na EU, nchi za EU zisaidie kupunguza changamoto kwa mataifa ya afrika mashariki wakati wa kufanya biashara, pamoja na kuhakikisha bidhaa za umoja wa afrika mashariki zinaingia Ulaya bila vikwazo.
                                     

Pamoja na mataifa haya kuwa nchi mwanachama wa EAC, mataifa mwanachama yanatofautia katika baadhi ya masuala ya uendeshaji wan chi yake, hivyo Tanzania ilikubali kusaini baada ya bidhaa za korosho na ngozi kukubali kuongezewa thamani tofauti na bidhaa nyingine za kibiashara.

Faida za mkataba huo ni kuanzisha mfuko wa EPA unaozitaka nchi za umoja wa ulaya kuchangia na kufidia hasara itakayozikumba nchi za umoja wa afrika mashariki ACP.
Nimemuuliza swali Balozi Kamala, nikitaka kujua changomoto kubwa kwa mataifa ya mataifa ya jumuhiya afrika mashariki.

Baadhi ya miradi inayotarajiwa kujengwa na mataifa ya EU afrika mashariki ni ujenzi wa reli kutoka dare s salaam, Isaka hadi Kigali Rwanda, reli ya tanga, arusha,moshi na  musoma Nchini Tanzania, kujenga vituo muhimu katika mipaka ya Tanzania na Zambia, pamoja na kuendeleza usafiri wa majini katika ziwa Victoria.

Hatahivyo kutokana na kila taifa kuwa na utaratibu wake, mkataba huu utazingatia matakwa na kufuata taratibu za nchi.

Na Mwanaharakati.

No comments: