Mafundi uashi wawili wamegundua
mabomu manane ya kutupwa kwa mkono ambayo inasemekana yamekuwepo ardhini kwa
Zaidi ya miaka 10 Kigoma kwenye Kijiji cha Mabamba walipokuwa wakichimba msingi
wa nyumba ya Mganga wa Kituo cha Afya.
Mafundi hao wamesema baada ya
kubaini kuwepo kwa chuma ambacho hawakukitambua waliamua kutoa taarifa Polisi
na Jeshi la Wananchi JWTZ, ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jafari
Mohamed amethibitisha kutoa kwa tukio hilo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment