Jumla ya wananchi 82506 walioko
halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Kagera wamejiandikisha kupiga kura katika
uchaguzi wa serikali za mkoani mitaa unaotarajia kufanyika Desemba 14 mwaka huu
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya
ya Biharamulo Bw Nassibu Mbagga amesema wananchi waliojiandikisha wamevuka
lengo la kuandikisha wapiga kura 79800 ambao walilengwa kuandikishwa katika
vituo 399 wilayani humo
Bw Mbagga mesema katika wagombea
waliojitokeza kutoka vyama vya CCM, CHADEMA CUF, TLP na
NCCR MAGEUZI kumetolewa pingamizi 18 lakini zimetupiliwa mbali kwa kukosa
vigezo halisi
Amesema katika uandikishaji huo na
kuwepo kwa wagombea wenyeviti wanne wa vijiji wamepita bila kupingwa
wengine ni wa vitongoji 49 wa CCM na wawili kutoka Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema)
Hata hivyoBw Mbagga
amewahimiza wananchi na wagombea kuendesha kampeni zenye ustaarabu kwa
kutanguliza sera zitakazokubalika na kulinda umoja wa kitaifa katika
kujipatia maendeleo na kukuza Demokrasia
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment