Serikali ya Tanzania imesainiana mkataba wa mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 45.21 na Shirika la
Maendeleo la Saudia kwa lengo la kuboresha miradi wa maji kwa wilaya ya Same,
Mwanga na ujenzi na ukarabati wa barabara Visiwani Zanzibar.
Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es
salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali ya Tanzania
na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas
Akiongea na waandishi wa habari katika
hafla hiyo, Waziri Saada alisema kuwa kati ya mkopo huo shilingi bilioni 41.25
ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia mradi wa maji
katika wilaya za Same na Mwanga na
shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi wa barabara Pemba, visiwani
Zanzibar.
Waziri Saada alilishukuru Shirika la
Maendeleo la Saudia kwa jitihada zao za kuisaidia Serikali ya Tanzania katika
kautatua tatizo la maji wilaya za Same na Mwanga pamoja na uboreshaji wa
barabara katika visiwa vya Pemba.
Aidha, mradi wa maji wa Same- Mwanga
utagharimu Dola za Kimarekani milioni 110.34 ambazo benki ya BADEA, Shirika la
Maendeleo Kuweit, OPEC na mashirika mengine wamekubali kukamilisha sehemu ya
fedha iliyobakia.
Mradi wa maji wa Same- Mwanga baada ya
kukamilika utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji vijijini amabapo
utasaida kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo, upatikanaji nwa
maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na kuboresha uchumi wao
kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda
mwingi kutafuta maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la
Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa makataba waliosaini
leo unaonesha kuwa Saudi Arabia iko mstari wa mbele katika kuendelea kuiunga
mkono Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake kwa kuzingatia mahusiano
mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa waandishi wa
habari na baadhi ya watumishi wa wizara ya Fedha na wawakilishi wa Serikali ya
Saudi Arabia.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment