Kutokana na meli ya Mv Victoria kukwama safari zake mara kwa
mara na kuzua mjadala na hasara kwa abiria na wafanyabiashara, waziri wa
uchukuzi HARISON MWAKYEMBE atimua uongozi mzima bandarini hapo na kuteua wapya.
Waliofukuzwa kazi ni Meneja mkuu Projest Kaija, na nafasi
yake imechukuliwa na Fabian Mayenga.
Kaimu mhasibu mkuu Tito W.Mwambagi, nafasi yake kuchukuliwa
na Beatus R. Rugalabamu, kaimu meneja masoko biashara, ameondolewa Cpt Obeid
Nkongoki nafasi yake inachukuliwa na Cpt Winton Mwasa.
Aliyefukuzwa mwingine ni kaimu meneja wa tawi Mwanza Beatus
T. Mghamba na kuingia Bwana Philemoni Bagambilana, Kaimu tawi Kigoma
ameondolewa Bwana Abel Giliard na nafasi yake kuchukuliwa na Anthony Stephen,
huku kaimu mwanasheria na menejautumishi anakuwa Fabian Mayenga baada ya
kuondolewa Josephat Mshumbusi .
Meli hiyo imesimamishwa kutoa huduma ili ifanyiwe ukarabati
wa kina, baada ya kubainika kuwa uongozi uliokuwapo ulikuwa ukiweka spare fake,
na kusababisha adha kubwa kwa watumiaji.
Waliopewa onyo sima kwenye picha hii chini.
Uongozi mpya umeanza kazi tangu tarehe 18 Dec 2014.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment