MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 17 December 2014

WAKURUGENZI WATANO WA HALMASHAURI WAFUKUZWA KAZI KWA KUVURUGA UCHAGUZI



Akithibitisha kusimamishwa kazi kwa Wakurugenzi hao,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Mh. Hawa Ghasia amesema kwamba
Wakurugenzi hao wametenda makosa yanayowaondolea sifa za kuwa Wakurugenzi.


“Makosa yafuatayo ndio yanayopelekea Wakurugenzi hawa kusimamishwa;Kuchelewa kuandaa vifaa vya kupiga kura,kukosa umakini katika kuandaa vifaa hasa karatasi za kupigia kura,kuchelewa kupeleka
vifaa kwenye vituo vya kupigia kura,uzembe katika kutekeleza majukumu yao pamoja na kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maandalizi ya uchaguzi kuwa yamekamilika huku wakijua kuwa siyo kweli”,alisema Ghasia


Aidha,Mh.Ghasia ameridhishwa na hatua ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumchukulia hatua mtumishi wake aliyemsingizia Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali na kusema ni jambo baya kutenda kosa na kusingizia watu au ofisi zisizohusika.

Wakurugenzi wanaosimamishwa kazi na kupisha uchunguzi zaidi ni pamoja na


Bw.Felix T.Mabula-Halmashauri
ya Hanang
Bw.Fortunatus Fwema-
Halmashauri ya  Mbulu


Bi.Isabela D.Chilumba- Halmashauri
ya  Ulanga


Bi.Pendo Malabeja- Halmashauri
ya  Kwimba
Bw.William
Z.Shimweta-Sumbawanga Manispaa


Pia, Mh.Hawa  Ghasia amesema Wakurugenzi wengine watatu(3)
wanapewa onyo kali na watakuwa chini ya uangalizi kubaini kama
wana udhaifu mwingine ili wachukuliwe hatua zaidi Wakurugenzi hao ni:-

        
Bw.Mohamed  A.Maje-Halmashauri ya Rombo


Bw.Hamis Yuna- Halmashauri ya
Busege


Bw.Jovin A.Jungu- Halmashauri
ya Muheza


Na Mwanaharakati.

No comments: