Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta
Luizer Mbutu amethibitisha kuwa Aisha amefariki dunia na alifia nyumbani kwao
sababu ambazo bado hazijafahamika.
Akizunumza kwa masikitiko Mbutu
alisema kwamba mwili wa merehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
“Hapa nilipo natetemeka kwa msiba
huu sababu marehemu alikuwa mzima na leo ndiyo ilikuwa aanze mazoezi na bendi
ya Twanga Pepeta kwa ajili ya maandalizi ya onyesho la maadhimisho ya miaka 16
ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta” alisema Luizer.
Aliongeza kwa kusema: "Hapa
natetemeka siamini lakini mwili nimeuona ni kweli Aisha amefariki na
amefikishwa hapa hospitalini akiwa tayari amefariki.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa bendi ya
Twanga Pepeta Asha Baraka pia amethibitisha habari hizo na hivi sasa yuko
njiani kurejea Dar es salaam kwa ndege akitokea Kigoma ambako alikwenda kwa
shughuli za uchaguzi wa serikali za mitaa.
Msiba uko Kigamboni maeneo ya Mikadi
Beach .
Aliyekuwa mnengua hodari wa African Stars band
"Twanga Pepeta" na Extra Bongo Aisha madinda enzi za uhai wake.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment