MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 12 December 2014

CCM WALALAMIKIA ESCROW KUWAPA WAKATI MGUMU GEITA

 





Katika mkutano wake uliofanyika (juzi)kwenye uwanja wa soko la mtaa wa mkoani mjini Geita,uliokuwa uhutubiwe na mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Geita Vicky Kamata kabla ya kushindwa kufika,baadhi ya viongozi wa chama hicho walijikuta wakiwa peke yao na wanachama wao wachache wenye sare za chama hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa mtaa wa mkoani waliokutwa wakifanya shughuli zao bila kusogea katika mkutano huo walidai kuwa hawaoni sababu ya kuwasikiliza wanaCCM kwa kuwa Rais Kikwete haoneshi nia ya dhati kuwawajibisha watuhumiwa wa Escrow.

''Ndugu yangu kwa hali ilivyo hapa nchini tumeamua hata tusihudhulie mikutano yao kabisa hawa watu ili wajifunze,yaani safari hii ni bora tuchague jiwe kutoka chama kingine na si chama cha mapinduzi,tumechoka kaka’’alisema Mabula kaloli mkazi wa mtaa wa mkoani aliyekutwa akicheza karata na wenzake umbali wa zaidi ya mita 300 kutoka eneo la mkutano.

Mwingine ni Mayala Kubingwa aliyedai kuwa,wakati nchi inatimiza miaka 53 ya uhuru wa kutokuwa na uhuru hakuna mtanzania hususani wa Geita anayeweza kusherehekea miaka hiyo,wakati hakuna huduma za kijamii na kudai kuwa iwapo chama hicho kingekuwa na nia ya kuwakomboa watanzania kingenyonga mafisadi wote wa Escrow.

No comments: