Uchaguzi wa serikali za mitaa huko
Geita umefunguliwa kwa vurugu kubwa ambapo mkurugenzi wa siasa na uenezi wa
chama cha wananchi(CUF)katika kata ya Kagu wilayani Geita Fransisco
Kadimu(34)amenusurika kufa baada ya kukatwa mapanga kichwani na vidoleni na watu
wasiofahamika.
Kutokana na hali hiyo wananchi wa
eneo hilo walikasirishwa na kitendo hicho na kulazimika kupiga yowe kujikusanya
na baadaye waliamua kuvamia makazi ya watuhumiwa kisha kuyasambaza na kuchoma
moto moja ya pool table ya mtuhumiwa wa ukataji mapanga.
Tukio hilo limetokea usiku wa
kuamkia Desemba 14 saa 5 usiku katika kijiji cha Kinaki kata ya Nyawilimilwa
Wilayani Geita Katika mkoa wa Geita.
Akizungumza kwa taabu na Dunia
Kiganjani Blog akiwa katika hospitali ya Wilaya ya Geita Kadimu alidai kuwa
alikumbana na wakataji hao wakati akitokea kwa katibu wa chama chake anayeishi
kijijini hapo.
Alisema,akiwa ameivuka senta ndogo
ya Calfonia ndipo alipokutana na watu hao ambao aliwatambua kwa majina na sura
ambao bila huruma walianza kumkat akata mapanga kichwani na mikononi sambamba
na kumpiga kwa fimbo na marungu hali iliyopelekea kupoteza fahamu.
Alisema,alikuja kupata fahamu
baadaye na kujikuta amezungukwa na wananchi waliofika eneo hilo kufuatia mayowe
aliyopiga kabla ya kuzirai na ndipo walipomkimbiza katika hospitali ya Wilaya
ya Geita anakoendelea na matibabu.
Katika tukio hilo mbali na
kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za kichwani pia kidole chake kimoja cha
mkono wa kulia kilinyofolewa kwa panga na kubakia na ulemavu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
afisa mtendaji wa kijiji cha Nyawilimilwa Charles Kidingi alisema,baada ya
tukio hilo wananchi walihamasishana na kwenda kuvunja makazi ya watuhumiwa hao
pamoja na kuteketeza kwa moto pooltable la mmoja wa watuhumiwa hao.
Aliwataja watu wanaodaiwa kuhusika
na tukio hilo ambao ni makada wa CCM kijijini hapo kuwa ni pamoja na Mashiku
Ndezu,Deo Ndezu,na wengine waliofahamika kwa jina moja la Raulian na Alex ambao
wamekimbilia kusikojulikana.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment