Makamanda wa Polisi pamoja na kikosi
cha OFM wakiwataiti wanawke waliokuwa wakijiuza.Ni aibu iliyoje! Tabia ya
wanawake kujiuza kwa kisingizio cha kusaka fedha kwa ajili ya Sikukuu ya
Krismasi imewatokea puani wanawake zaidi ya kumi akiwemo mke wa mtu baada ya
kunaswa mawindoni na kutiwa nguvuni.
Tukio hilo la aibu lilitokea katika
msako maalum wa polisi waliotoa kolabo kwa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya
Global Publishers, uliofanyika katika eneo ‘korofi’ la ltinga, Msamvu Kata ya
Mwembesongo mkoani hapa, wikiendi iliyopita.
Wanawake
hao wakiwa chini ya ulinzi mkali. Awali, Kamanda wa OFM mkoani hapa alipokea
malalamiko lukuki kutoka kwa wananchi waishio jirani na eneo hilo waliokuwa
wakiwalalamikia wanawake hao kugeuza vibanda vyao vya simu kuwa gesti na
kuvitumia kufanyia ngono usiku na kuzagaa kwa kondom kila sehemu.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment