Hekaheka ya leo December 11
inatoka Tanga, ambapo jamaa mmoja mwenyeji wa Tabora alikwenda huko kwa
lengo la kuoa na baada ya kuoa akakutana na mauzauza ya ajabu hali iliyomfanya
mpaka sasa hali yake kiafya kuwa sio nzuri.
Bwana huyo amesema siku ya Jumapili
alikwenda nyumbani kwa wakwe zake kuaga lakini akiwa njini kurudi alikutana na
msichana mdogo akitokea mbele yake lakini kadri walivyokuwa wakikaribiana
msichana huyo alizidi kuwa mrefu, akataka kugeuka kukimbia ambapo akakuta kuna
watu wengine wawili nyuma yake ambao walimwagia maji akapoteza fahamu.
Baada ya kuzinduka alijikuta
amewekwa sehemu huku waliomzunguka wakijadiliana kumkata ulimi na wengine
wakipingana na mawazo hayo, baadaye walimpeleka kwenye mti na kumlazimisha ale
nyama ambayo hakujua ni nyama ya nini kisha wakampeleka baharini ambako kulikuwa
kumewekwa sherehe nako walitaka kumkata ulimi pia akakataa ambapo kati ya watu
hao wapo waliokuwa wakikataa pia kumkata ulimi.
Alifanikiwa kuwasiliana na ndugu
zake kwa njia ya message mpaka wakafika mahali ambapo watu hao walimuacha,
anasema kwamba anawatambua watu wote waliokuwa wakimfanyia mauzauza hayo japo
amegoma kuwataja kwa mke wake.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment