Ni katika kipindi cha miezi miwili tu, kuanzia octoba 9 hadi
Desemba 4 mwaka huu, ambapo jumla ya vijana 6 wameuawa katika mazingira ya kutatanisha, watatu wamechinjwa katika kata ya Kitendaguro,
1 katika kata ya Rwamishenye, huku wawili wakichinjwa katika kata ya Kibeta ndani
ya manispaa, huku wananchi wakishangaa ukimya wa mamlaka bila kuchukua hatua.
![]() |
| Kanisani alipouawa mwalimu Ng"wandu |
Tarehe 09 october, alieuawa mwalimu DIONIZ NGW’ANDU wa shule
ya sekondari Kagemu, alipokuwa katika kanisa la PAGT, baada ya kukatwa kichwa
na kitu chenye ncha kali, huku jamaa yake aliyekuwa mlinzi katika kanisa hilo
siku hiyo akijulikana kwa jina mojala THEMISTOCRES akisalia na ulemavu wa
maisha, kama alivyoeleza mchungaji wa
kanisa hilo FAUSTINE JOSEPH.
Siku kati ya 5 au saba badaye, mwili wa kijana ambaye
hakutambuliwa majina wala sura, ulikutwa umeharibiwa kwa kunyofolewa macho, huku
ukitupwa kando mwa shamba la mmoja wa wakazi wa Kitendaguro, ambapo Anakret Laurent Kyaishozi miaka 30 alikuwa
shuuda, aliueleza mtandao huu kuwa mwilihuoulichukuliwa na polisi mpaka sasa
hawajajua ninikiliendelea.
Kando na hayo, familia ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka
37 Erick Kashaga akiacha mjane Sofia Mozes miaka 32 na watoto saba, imesalia
katika mvutano mkubwa,na familia ya bwana Levocatus , ambaye mpaka sasa yuko
mikononi mwa jeshi la polisi, huku jamaa zake wakielezwa kuwa uchunguzi
unaendelea.
![]() |
| Kaburi la Mozes Kashaga |
![]() |
| Mzee Rumumba akionesha eneo alipochinjwa Mozes |
Mzee SILIDION RUMUMBA mwenye umri wa miaka 73, ndiye mmiliki wa kilabu cha pombe, ambacho
dakika za mwisho marehemu aliondoka hapo muda wa saa tano usiku, akiwa na jamaa
zake wawili.
Ndani ya dk kama mbili baadaye, liyetajwa kwa jina moja tu
la Eriki alirudi nyumbani kwa mzee SILIDION RUMUMBA akiwaeleza kuwa wamevamiwa
na mtu ambaye alimtaja jina, huku akisema kuwa hana hakika kama watamkuta hai
Kashaga, ilhali akitoa taarifa hizo kimyakimya, pasi na kupiga kelele wakati wa
tukio,jambo ambalo linawashangaza wengi, kwasababu marehemu ameuawa karibu
kabisa na makaazi ya watu.
![]() |
| Mama mzazi wa Mozes |
Kando na maelezo hayo, nimetaka kusikiliza ushuuda wa Erick aliyethibitisha
kuwa alishuudia mauaji hayo, lakini nyumbani kwaojamaa zakewalisema kuwa huwezi
kumwona sababau wamemficha sehemu baada ya kutishiwa na mkewa mtuhumiwa.
Hayo yamesalia katika familia hizo ndani ya kata ya
Kitendaguro, huku katika kata ya kibeta, lawama kubwa zikiangushwa kwa mamlaka,
kuwa hawajaonesha juhudi zozote baada ya
kuuawa kijana GOODRUCK FRANCIS aliyekuwa na umri wa miaka 38, ambapo taarifa za awali zinaonesha kuwa aliuawa kwa
kukatwa shingo na watu wasiojulikana, ikiwa ni kando kando mwa barabara ya mtaa
wa Kibeta Amjuju.
Bi Stella Lenatus amesema amekata tama kwasababu tangu
ahojiwe, ameenda kituoni kujua taarifa za mdodgo wake na kuambiwa asubiri
walikuwa bize na kazi nyingine muhimu.
![]() |
| Hapo kustoto pichani ndipo aliuawa Gudrack eneo la Kibeta Anyama. |
Sambamba na wanaouawa pasipo kutambulika majina na makwao
ndani ya manispaa ya Bukoba, Ernest Kato ni kijana aliyeuawa mwezi novemba
akiwa na miaka32,katika mtaa wa Bugezi kata Rwamishenye, majira ya usiku, na
kutambulika asubuhi ya tarehe iliofuata kwa kukutwa amechinjwa, huku akiacha
mjane na mtoto mmoja, ambaye hatahivyo
amekimbia kwa kuhofia naye kuawa.
Mmoja kati ya wanafamilia wa marehemu Ernest, ameomba jina
lake lihifadhiwe, pamoja na kusema kuwa wanaishi kwa hofu kubwa kiasi cha
kujipangia muda wa kurudi nyumbani mapema nyakati za usiku, na shughuli
zimesimama.
Mauaji ya mwisho hadi
ninakamilisha makala haya, ni alivyouawa Joran Rutulaniisa, mkaazi wa Kibeta
magoti, nilifika eneo la tukio muda mfupi tu baada ya polisi kuubeba mwili wake
lakini taarifa za ndugu ambao hatahivyo wanahofu ya maisha yao, ni kuwa
nduguyao ameuawa kwa aina ile ile ya
vifo vya kukatwa koromeo.
![]() |
| Marehemu Rutu enzi za uhai wake |
Tetesi ambazo bado sijazithibisha, wananchi wanaofanya biashara
ya senene, wamelazimika kuanza kujifunga vitu vigumu na tauro shingoni, kama
taadhali watakapovamiwa.
![]() |
| Shangazi na mama mdogo wa marehemu kwenye kaburi la Rutu |
![]() |
| Baba wa marehemu Rutulanisa |
Mauaji nikitendo kisichokubalika kwa mwenyezi Mungu, jambo
linalompa shekh mkuu wa mkoa wa Kagera Aruna Kichwabuta,kukemea hali hiyo
katika mamlaka na wananchi.
![]() |
| Shekh mkuu wa mkoa Aruna KICHWABUTA |
Makala maalumu sehemu ya kwanza kuhusu mauaji hayo inaruka
marudio leo saa moja jioni kupitia 88.5 Kasibante fm Bukoba.
Na Mwanaharakati.









No comments:
Post a Comment