Ugonjwa huo ulianzia mkoani Kagera mwaka 1983 wilayani Misenyi katika kata ya Kanyigo, ambapo Wananchi mkoani Kagera wanaadhimisha siku hiyo huku kiwango cha ugonjwa huo kikionesha kupanda hadi 4.8% mkoani humo,kutokana na sababu zilizotanjwa kuwa wamejisahau baada ya mashirika na taasisi kwa kushirikiana na wananchi kukomesha UKIMWI miaka ya nyuma kufikia 2010.
Mratibu wa
UKIMWI mkoani Kagera kupitia taasisi ya kupambana na kudhibiti UKIMWI, Bi Jeneviva
Emmanuel amesema kuwa TACAIDS kwasasa imeamua kushirikisha asasi mbalimbali za
serikali na zisizo za kiserikali ili kuona kama itaweza kukabiliana na kuanza
kupanda kwa kiwango hicho cha maambukizi, akitaja wakati wa miaka ya themanini kuwa
kiwango cha maambukizi kilifikia 19% ambapo jitihada zilizofanywa na wahisani
zilipunguza maambukizi hayo hadi 3.4% kufikia mwaka 2011.
Na Eddy Blog, Njombe
Wananchi mkoani Njombe wameaswa
kutoliingiza suala la tohara ya wanaume na imani za dini kwa kuwa suala hilo ni
kwa ajili ya kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na manufaa
mengine ya kiafya na si vinginevyo
Hayo yamebainika wakati wa
uchangiaji mada iliyowasilishwa katika kikao cha wadau wa mapambano dhidi ya
vvu kilichoandaliwa na tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) ambapo
imeonekana miongoni mwa changamoto ambayo shirika la JHPIEGO lilikutana nayo
wakati wa utekelezaji wa huduma ya tohara ya wanaume ni imani ya dini
Mmoja wa wachangiaji hao askofu
mstaafu Dkt Peter Lukumbusho Mwamasika ameeleza kuwa wapo baadhi ya watu
wanadai wanaume wakifanyiwa tohara wanakuwa wamehamishwa katika imani yao ya
kikristo na kupelekwa katika imani ya kiislamu jambo ambalo limepingwa vikali
kuwa halina ukweli wowote
Askofu huyo amesema katika kipindi
hiki ambacho kila mmoja anapambana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi,
tohara imegundulika kuwa ni moja ya njia inayopunguza kasi ya maambukizi ya
virusi vya ukimwi kwa waliofanyiwa tohara hivyo mwanaume aliyefanyiwa tohara
imani yake ya dini inabakia pale pale
Kwa upande wake mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayoshughulikia
Ukimwi Mh. Lediana Mng'ong'o amewataka viongozi wa siasa kushirikishwa katika
jitihada za kupambana na maambukizi ya VVU
"Humu ndani siwaoni madiwani,
siwaoni wenyeviti wa halmashauri, angalau nawaona wakuu wa wilaya, wenyeviti wa
halmashauri ndio wasimamizi wa sheria ndogondogo ninaomba tuwashirikishe sana
maana wanaushawishi mkubwa katika hili" amesema Mng'ong'o
Amesema kwa nafasi hii
wakishirikishwa viongozi wa siasa watakuwa wanapeleka taarifa hizo kwa wapiga
kura wao suala hilo litasaidia kuwa na mabadiliko makubwa katika jamii
Maadhimishoya
siku ya UKIMWI Duniani,kimkoa yanafanyika wilayani Biharamulo, kitaifa
yanafanyika mkoani Njombe, ambao
unaongoza kwa maambukizi kitaifa kwa asilimia 14.8 huku Pemba ikiwa chini ya
asilimia 1.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment