Meneja wa Radio Kahama FM Marco Mipawa amevifahamisha vyombo vya habari nchini kwamba, yeye pamoja na washiriki wenzake 8, wamekubali kwamba kuna umuhimu wa kufanyika mabadiliko makubwa katika sekta ya habari nchni, ili iwe kama ilivyo nchini Ghana.
Kwa upande wake Mipawa amekiri kufurahishwa na uhuru wa vyombo vya habari nchini Ghana, ambapo huwa vinafanya shughuli zake kwa uhuru mkubwa katika uibuaji wa agenda za kuzuia uovu dhidi ya serikali bila vitisho vyovyote.
Meneja wa Jogoo FM Radio ya mjini Songea Magira Magira amejifunza umuhimu wa kutazama kipaji cha mtu katika utangazaji ili jamii imkubali, na kwamba elimu ni kitu cha ziada katika kusaidi kukilinda na kukiboresha kipaji hicho.
Naye Meneja Masoko na Mhasibu wa Kahama FM Radio ya mjini Kahama Leticia Kagoro amesema, alichojifunza ni umuhimu wa kuwekeza katika raslimali watu na vitu, kabla ya kuanza uendeshaji wa mradi wowote ikiwemo miradi ya Redio.
Amekiri kwamba, mafanikio yanaweza kufikiwa kwa kuweka malengo ya muda mfupi na mrefu yanayopimika katika uendeshaji wa redio, tv na vyombo vingine; ili kuwa na mwongozo katika utekelezaji wa kazi na tathmini yake.
Wakati huohuo, mkuu wa msafara huo na mmiliki wa Radio CG FM kutoka Tabora Charles George, amewaasa wamiliki na waajiri wa Redio kutambua vipaji vya watumishi wao kabla ya kuwaajiri, kuviendeleza na kuvilinda kwa gharama yoyote.
Naye mwandishi kutoka Triple A FM ya mjini Arusha Marick Munga amesema, alichojifunza ni umuhimu wa vyombo vya habari kufanya tafiti za kina kwa jamii ili kubaini mahitaji yake kabla ya kuibua agenda zinazoihusu.
Meneja wa Standar Radio iliyoko mjini Singida Alice Achieng amefurahishwa na tabia ya ushirikiano wa wafanyakazi katika vipindi mbalimbali redioni na televisheni,ambapo kwa kila kipindi daima huwa pamoja ili kuhakikisha wamepeleka ujumbe ambao jamiia inauhitaji
Timu hiyo ya wanahabari kutoka Tanzania nchini Ghana, jana imemaliza program ya kutembelea kituo cha Multimedia Group LTD kilichoko jijini Accra, ambapo wiki ijayo itatembelea vituo vingine vya habari mjini Kumasi nchini humo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment