MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa
Morogoro jana ilishindwa kuanza kusikiliza kesi ya Katibu wa Jumuiya ya
Waislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda kutokana na mgongano wa kiutawala na
kukosekana kwa nakala ya hukumu ya rufaa iliyompa ushindi Mahakama Kuu ya
Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
Kesi ya Ponda ilishindwa kuanza
kusikilizwa mahakamani hapo kufuatia kushindwa kufikishwa kwake
kulikosababishwa na kusigana kwa tarehe iliyopangwa kwenye jalada la kesi hiyo
ambayo ni Desemba 8, mwaka huu, na ile ya amri ya kutolewa rumande ya Gereza la
Morogoro kwa uongozi wa Jeshi la Magereza ikiwa imeandikwa akitakiwa kuondolewa
Desemba 10, mwaka huu ili kufikishwa Mahakamani.
Katika kikao hicho, upande wa
mashikata ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Sunday Hyera, sambamba
na maofisa wa Mashikata wa Polisi, wakati kwa upande wa utetezi wa Ponda,
uliwakilishwa na Wakili Bartholomew Tarimo.
Hata hivyo baada ya kumaliza
majadiliano hayo mafupi Mahakamani hapo, Wakili Tarimo, aliwaambia waandishi wa
habari kuwa kumetokea tofauti ambayo imesababishwa Ponda kushindwa kufikishwa
mahakamani hapo.
Kwa mujibu wa Wakili huyo wa
utetezi, kusigana huko ni kwa tarehe ya hati iliyotolewa kwa Jeshi la Magereza
kuhusu kuletwa Ponda Mahakamani hapo ikiwa ni tofauti na uliyopo katika jalada
la kesi yake.
Hivyo alisema kuwa, jalada la kesi
hiyo limeandikwa siku ya Desemba 8, mwaka huu kuwa mshikatiwa afikishwe
mahahakamani, ikiwa ni tofauti na waliyopelekewa Magereza ya kuletwa kwake
mahakamani kuwa ni Desemba 10, mwaka huu.
Pia alisema upande wa utetezi
sambamba na wa Jamhuri pamoja ulifikia uamuzi wa kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi
Desemba 22, mwaka huu kutokana na kutokuwepo mahakamani hapo nakala ya hukumu
ya rufaa ya kesi aliyoshinda Shehe Ponda iliyotoka Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar
es Salaam iliyompa ushindi akipinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya
Kisutu.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment