|
Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri
Mkuu-TAMISEMI, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wanahabari
|
Idadi hiyo ni sawa an asilimia 97 ya
wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa waandishi wa habari leo
imesema ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na mwaka jana.
Hata hivyo, jumla ya wanafunzi 12,
432 waliofaulu, hawajapata nafasi ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ay
sekondari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uungufu wa majengi, hali
inayowalazimisha kusubiri chaguo la pili litakalofanyika mapema mwakani.
Jumla ya wanafunzi 808,085
walisajiliwa kufanya mtihani wa taifa mwaka 2014 lakini ni wanafunzi 792,122 tu
ndio waliofanya mtihani, hiyo ikiwa ni asilimia 98.02% ya wanafunzi wote
waliosajiliwa.
Taarifa ya Tamisemi inaongeza kuwa
wavulana wanaongoza kwa kuchagaliwa zaidi ya wasichana ambapo jumla ya wavulana
219,964 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hiyo ikiwa ni sawa na
asilimia 97.28 ya wanafunzi wote waliochaguliwa huku wasichana wakifikia
218,996 ambayo ni sawa asilimia 97.1 ya wanafunzi waliochaguliwa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment