Kamanda wa polisi mkoani Kagera Henry
Mwaibambe, amesema kuwa sasa wameanza doria kaliambayo inahusisha maeneo yote
muhimu na yenye taarifa za mauaji,huku watu watatu wameshakamatwa kuhusiana na
mauaji katika manispaa ya Bukoba.


Kamanda Mwaibambe, amekiri kuwapo kwa
mauaji ya kutatanisha, alipoongea na mwandishi wa habari hii ya uchunguzi
Nicolaus Mac Ngaiza, kuhusu mauaji ya kutatanisha manispaa ya Bukoba, huku
akisema kuwa polisi haiwezi kuficha huku wananchi wakipoteza maisha na kuishi
bila amani.
Amesema kuwa kutokana na rekodi za vifo
kuanzia October 6 hadi December 5 2014, kama makala ya mwandishi inavyosema,
wamepitia taarifa zao na kugundua kuna vifo vya watu saba vya kufanana ambavyo
hatahivyo haviusiani na imani za kishirikina, kwani hakuna kiungo
kinachoondolewa baada ya mtu kuuawa.
ACP Mwaibambe, amewataja waliouawa kuwa
ni Mwl Ng’wandu, Mozes Kashaga, Ernest Kato, Goodrack Francis, Rutu, na vijana
wawili ambao hawakutambulika, majina mmoja akikutwa kwenye shamba la mwananchi
mmoja Kitendaguro,hukumwingine akikutwa kwenye Bwawa la maji kata
Kashai,ilhaliakiwa na jeraha la kukatwa na kitu cha ncha kali kichwani.
Amewataka wananchi kuviamini vyombo vya
dola, hukuakiongeza kuwa watakuwa wakiwajulisha wananchi kila kinachoendelea
lakini akawaomba kusaidia jeshi hilo kufichua wahusika na kusema kuwa sasa
wanazweza kuendelea shughuli zao za kibiashara tofauti na kujifungia saa za
jioni kuhofia maisha yao.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment