Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni na
Michezo Juma Nkamia amenusurika kupigwa na wananchi jimboni kwake baada
ya kutoa kauli zenye kejeli.


Nkamia ambae pia ni Mbunge wa Kondoa
Kusini alikumbwa na hali hiyo wiki iliyopita alipokua katika kijiji cha Nchemba
alipokwenda kuwanadi wagombea wa CCM katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za
Mitaa uliofanyika wiki iliyopita.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho
alisema Nkamia aliponzwa na kauli za kejeli alizozitoa dhidi ya aliyekua
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Msongozli Yahaya kutoka CUF.
Mkamia alimtuhumu Mwenyekiti huyo
kwamba amekua akimchafulia mbele ya wananchi wake kwa lengo la
kumkwamisha katika uchaguzi ujao”Pamoja na kutoa maneno mengi ya kejeli hali ya
hewa ilianza kuchafuka pale ambapo Nkamia alipoagiza wasaidizi wake wamkamate
mwenyekiti huyo aliyekua amekaa pembeni na kumpeleka katika gari lake.
Baada ya hali hiyo wananachi
walianza kuzunguka gari la Nkamia huku wakiwa na mawe ili kuhakikisha
Mwenyekiti wao hakamatwi huku Nkamia akilizimika kuingia ndani ya gari na
kuondoka kwa hofu ya kupigwa.
Na:gazeti la mtanzania
No comments:
Post a Comment