Zaidi ya watui arobaini wamenusurika
kifo huku mmoja akikatika viungo vya miguu na wengine kujeruhiwa vibaya
baada ya lori moja lilioonekana kuwa ni la jeshi kugongana uso kwa uso na
gari la abiria aina ya COSTA la ubungo Tegeta eneo la Tegeta jijini Dar es
salaam.
Mamia ya wakazi wa Tegeta wamefurika,
huku baadhi ya mafundi gerejji wa Tegeta wakijaribu kutumia vifaa maalumu
kukata mabati ya magari kwa nia ya kunasua baadhi ya majeruhi walionasa ndani
ya COASTA hiyo kusuru abiria walioonekana kunasa katika vyuma vya magari hayo
baadhi ya mashuhuda na Dereva wa COSTA pamoja na kuomba eneo la kibaoni kuweka
njia ya mzunguko maarufu kama ROUND ABOUT kwa lengo la kuepusha madereva wanao
lazimika kugeuza kwa dharura katika njia kuu kutokana na njia hiyo kukosa fursa
ya kugeuza endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo pia wamemtupia lawama Dereva wa
Lori kama msababisha ajali kwa kukosa hekima ya kuchukua tahadhari kabla ya
kufanya hivyo.
Kamanda wa polisi mkoa kipolisi
kinondoni Kamilius Wambura amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza
kutoa taarifa mara baada ya uchunguzi kufanyika.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment