MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 29 January 2015

BREAKING NEWS!!! BOAT YASADIKIWA KUZAMA NA WATU WANAOSADIKIWA KUFIKIA 30 HUKU NYUMBA KADHAA ZIKIEZULIWA KWA UPEPO MKALI KAGERA

Ni katika kata ya Goziba kiwani Goziba wilayani Muleba, ambapo taarifa za awali zinasema kuwa umezuka upepo mkalisaa nne leoasubuhi, na kuezua nyumba za wafanyabiashara, makaazi, kituo cha polisi na hema la shirika ICAP la kutolea huduma za kiafya kwa kina mama.

Mtendaji wa kata hiyo Bwana Nason Bahemka aliyezungumza na mtandao huu hivi punde amesema kuwa kulikuwa na Boat inayofanya safari zake kutoka Goziba kwenda Ukerewe, inasadikiwa kuzama huku ikiwa na watu zaidi ya 30 ambao hakuna ambaye ameonekana mpaka sasa hivi, huku wakiendelea kufanya mawasiliano.

Amesema kuwa kisiwa hicho chenye wakaazi zaidi ya elfu 7 wengiwao wamejeruhiwa kwa kukatwa na mabati ya nyumba zilizoezuliwa ikiwamo ofisi ya kijiji na mtoto mmoja yuko mahututi.

Mtendaji wa kijiji ametajwa kuwa anaumwa na amelazwa hospitali ya Rubya. tunaendelea kufanya nmawasiliano zaidi kutuletee undani. 
Na Mwanaharakati.

No comments: