TAARIFA
KWA UMMA
Kuna
uvumi unazagaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii kuwa mmiliki wa VIP
Enginering and Marketing Limited, “aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu
Rugemalira” amefungua kesi Mahakama Kuu akiidai Serikali jumla ya TShs. 398
bilioni.
VIP
Engineering and Marketing Limited inapenda kuufahamisha umma kuwa hizi taarifa
si za kweli, hakuna kesi yoyote ambayo imefunguliwa na VIP Engineering and
Marketing Limited au Bw. James Rugemalira dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Mahakama Kuu ya Tanzania au Mahakama nyingine
yoyote.
VIP
Engineering and Marketing Limited inaamini uvumi huu unalenga kuleta
uchonganishi wa VIP Engineering and Marketing Limited kwa umma ili kukidhi
maslahi binafsi ya waanzilishi wa uvumi huo.
VIP
ENGINEERING AND MARKETING LIMITED
03
JANUARI, 2015
Email:
vipemltd2@gmail.com
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment