MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday 28 January 2015

BREAKING NEWS!!! WANANCHI WAVAMIA GARI LA ZIMAMOTO KWA KUCHELEWA KUFIKA ENEO LA TUKIO, TUKIO LINGINE CLUB YAUNGUA DAR TAZAMA PICHA MBALIMBALI

CLUB Olympia iliyoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam, imeungua na kuteketea kwa moto majira ya saa kumi na nusu usiku wa kuamkia leo ambapo chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mapema.

Mlinzi wa club hiyo inayomilikiwa na Samuel Mwaisumbe, na ambaye hakuweza kujitambulisha jina lake, alisema moto huo ulianza mishale ya saa kumi usiku ambapo waliweza kutoa taarifa kwa vyombo vya zima moto.

Aliongeza kwamba zima moto hawakufika kwa muda mwafaka na badala yake walifika kunako saa 12 asubuhi wakiwa na maji kidogo ambayo yaliisha wakati moto ukiendelea.


Vyumba zaidi ya kumi na nne vimeteketea kwa moto maeneo ya Mwananyamala Manjunju kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni hitalifu ya umeme ambapo licha ya jitihada za wananchi za kuuzima moto na kuokoa vitu kutokuzaa matunda mamia ya wakazi wa eneo hilo wamelivamia gari la zima moto kwa madai kuwa limechelewa kufika katika eneo hilo.Fuatilia Taarifa zetu Kufahamu zaidi.
Na Mwanaharakati.

No comments: