SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda ameliahirisha Bunge hadi kesho baada ya
kutokea mabishano kufuatia hoja iliyowasilishwa na Mhe. James Mbatia akitaka
kujua hatma ya Vurugu zilizotokea jana mara baada ya kukamatwa
kwa wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa
chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali.
Mbatia aliomba suala hilo lijadiliwe na Bunge kama suala la dharula, asubuhi, Spika akaahirisha hadi jioni, lakini jioni akatoa taarifa za kuahirisha hadi kesho.
Mwongozo waSpika alioutoa :- Alisema kuwa Kutokana na unyeti na udharula wa suala hilo, basi Serikali ilete majibu kesho bungeni na taarifa ya kilichojiri jana ili bunge lipate fursa ya kujadili.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo ya Spika ilionekana dhahiri wabunge wa upinzani kupitia umoja wao wa UKAWA hawakuridhishwa na hayo maelezo, ndipo walipoamua kusimama na kwa kauli moja wakipaza sauti zao wakisema shughuli za bunge haziwezi kuendelea mpaka hoja yao ya msingi ipate majibu.
Hali haikuwa shwari ndipo Spika wa bunge Mhe. Makinda akafanya maamuzi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment