![]() |
Marehemu WP Judith |
![]() |
Marehemu Cop. Edgar |
Majambazi yaliyojihamu kwa silaha
yamevamia Kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua askari
wawili na kupora silaha zilizokuwepo kituoni hapo.
Tukio hilo limetokea usiku wa
kuamkia jana, huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa
mapanga na WP Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea
upande wa kushoto.
Jana watu walikusanyika huku polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika
tukio la uvamizi, kituo cha polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani.
Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2,
SHORTGUN 1, silaha 2 za mabomu ya machozi na risasi 60 za SMG.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment