Ni binti wa darasa la 7 Antia Hildephonce mwenye umriwa
miaka 13, aliyekabwa na mfupa wa samaki akiwa darasa la tatu shule ya msingi
Kibeta Bukoba mjini, ambapo inadaiwa wakati wote alikuwa akisikia maumivu kwa
msimu.
Ametapika mfupa huo pichani pamoja na vipande vya minofu
isiyoeleweka ni ya nyama gani pamoja na uchafu mwingine, huku akisema kabla ya
kutapika alivimba tezi kwa muda wa siku tatu huku homa kali ikimshika na baada
ya kutapika sasa anajisikia vizuri.
Ameuambia mtandao huu kuwa, alitunza siri ya maumivu yake
kwasababu aliwahi kumweleza mama yake Winifrida Mlama, kuwa alikabwa na mfupaa na wakati huo, ndipo mama yake
akamkaripia na kutishia kumchapa hivyo akaogopa kusema hata wakati maumivu
yalivyokuwa yakimsumbua anaamua kunyamaza.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment