MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 20 January 2015

MFANYABIASHARA BI RUGEIYAMU AUAWA KWA RISASI





Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Prisca Paul Rugeiyamu au Mama Koku (34) ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi nje ya geti la nyumba yake huku mwanaye Careen (12) akishuhudia.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni majira ya saa mbili usiku maeneo ya Tabata Segerea, jijini Dar es Salaam, ambapo kwa mujibu wa chanzo, Prisca, alikuwa akirudi kutoka katika biashara zake.

Inadaiwa kuwa alipokuwa akisubiri kufunguliwa mlango, watu waolisadikiwa kuwa majambazi wakiwa na pikipiki walimzunguka na kumtaka kutoa fedha na laini anazozitumia katika huduma za fedha kwa njia ya simu katika maduka yake.

Hata hivyo marehemu alibishana kwa muda na majambazi hayo ambapo walimpiga risasi na mguu na kumuongeza nyingine ya tumboni na kumpora fedha zilizokadiliwa kuwa ni milioni 45.

Inadaiwa kuwa mtoto wake baada kushuhudia mama yake alipigwa risasi alikimbilia kwa kwa bibi yake ambaye yupo jirani na nyumbani kwao akiwaacha majambazi wakijiandaa kuondoka.

Inadaiwa kwa kusaidiana na majirani kumkimbiza Prisca, hospitali ya Amana, ambapo alifia njiani na maiti yake kuhifadhiwa katika hospitali hiyo.

Mmoja wa ndugu wa marehemu alisema kuwa katika jambo la kushangaza siku ya msiba wafanyabiashara wa madini walifika na kujitambulisha kuwa marehemu alikuwa mfanyabiashara mwenzao na kudai kuwa marahemu hakuweza kuliweka bayana.

Marehemu alikuwa akimiliki maduka ya jumla ya vocha, mfanyabiashara wa madini, duka la vinywaji na duka la vifaa vya ujenzi maeneo ya Tabata Segerea.
 


Na Mwanaharakati.

No comments: