
Wakizungumza
katika machinjio ya bukoba ambapo kwa siku ya leo wamesema kuwa hawawezi
kuchinja nyama yoyote mpaka wafikie muafaka na serikali wamesema kuwa majibu
yanayotoka katika mamlaka husika hayaridhisha katika upandishaji wa nyama.
Bwana
RASHID ISMAIL, HAKIMU HUSSEIN pamoja na
EDWINI PASTORI wamesema kuwa kukosekana kwa ngombe katika mkoa wa kagera
kunatokana na ngombe hao kuwa na soko kubwa katika baadhi ya nchi kama
COMORO,SUDAN UGANDA pamoja na nchi nyingine.
Aidha
wamesema kuwa kupanda kwa kitoweo hicho
kunasababishwa na mambo mengi ikiwemo kupandishiwa bei ya leseni pamoja na
mambo mengine na kuiomba serikali kitafarkari suala hilo kwa makini.
Kwa
uapnde wake mwenyekiti wa wachinjaji manispa ya bukoba bwana HATWIBU MUSA amesema kuwa
sababu zinazotolewa na serikali hazina mashiko kutokana na kiwango
kikubwa cha utoroshaji ngombe kwenda nje ya nchi.
Aidha
ameongeza kuwa usimamaji wa uchinjaji wa ngombe hautaendelea mpaka pale
wanatakapofikia muafaka kwani barua waliyoipokea jana inasema washushe kitoweo
bila ya hivyo wasifungue bucha zao.
Bwana
MUSA ameongeza kuwa awali walikaa na mkuu wa mkoa ambapo walikubaliana
kupandishwa kitoweo hicho lakini baadae
makubaliano hayo yamekiukwa.
Na Mwanaharakati.



No comments:
Post a Comment