Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwaarifu Wizara imeanza zoezi
la kuwapangia vituo vya vya kazi Wataalam wa Kada za Afya kwa mwaka wa fedha
2014/2015.
Wataalam
wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kwa waajiri wao ndani ya siku 14
tangu tarehe ya tangazo. Aidha,waajiri wanakumbushwa kuwasilisha taarifa kwa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu wataalam ambaohawajaripoti
ili kuona uwezekano wa kujaza nafasi zao.
Vilevile,
waajiri wanakumbushwa kukagua vyeti halisi vya kidato cha IV na VI, Vyeti vya
taaluma na vyeti vya usajili (kwa wataalam wenye masharti ya usajili kwa mujibu
wa miundo yao yau tumishi).
Orodha ya
majina ya wataalam waliopangiwa kazi pamoja vituowalivyopangiwa inapatikana
kwenye tovuti ya wizara www.moh.go.tz. Wizara haitatoa barua za kupangiwa vituo
vya kazi kama ilivyokuwa awali.
Nawapongeza
wataalam wote kwa kupata nafasi ya kutumia utaalam wenu katika kuwahudumiwa
wananchi, na ninawatakia kazi njema na utumishi uliotukuka.
Imetolewa na:-
Katibu Mkuu
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
06 Januari, 2015
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment