Pamoja na mambo mengine baadhi ya
mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-
1. SAKATA LA AKAUNTI
YA ESCROW
Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa
sana na sakata hili. Baada ya kulijadili kwa muda mrefu na kwa kina Kamati Kuu
imeamua yafuatayo:-,
i). Pamoja na yale ambayo
yameshatekelezwa na serikali, Kamati Kuu imeitaka serikali na vyombo
vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge juu ya swala hilo.
ii). Kamati Kuu imewataka wote
wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa dhamana zao, na
wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za kuwawajibisha.
iii). Aidha Kamati Kuu imeiagiza
Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili kwa wale wote waliohusika
na ukiukwaji wa maadili kwenye sakata la Escrow na wako kwenye vikao vya
maamuzi vya Chama. Kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili kitafanyika tarehe
19/01/2015 kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.
2. WALIOPEWA ADHABU KWA
KUKIUKA MAADILI YA CHAMA.
Itakumbukwa kuna makada sita wa CCM
walipewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa
kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais, watamaliza muda wa adhabu zao mwezi wa
pili mwaka 2015.
Baada ya muda wa adhabu zao kuisha,
itafanyika tathimini kuona kama walizingatia mashariti ya adhabu zao. Na kama
kuna ambao watakutwa hawakuzingatia mashariti ya adhabu zao wataongezewa
adhabu.
3. SOKO LA MAHINDI
Kamati Kuu imepokea taarifa ya
mwenendo wa soko la mahindi nchini. Baada ya tathimini na uchambuzi,
pamoja na kazi iliyofanywa na serikali, Kamati Kuu imeiagiza serikali
kuangalia upya mfumo unaotumiwa na Hifadhi ya Taifa ya Chakula ( NFRA)katika
ununuzi wa mahindi, ili unufaishe zaidi wakulima badala ya utaratibu wa sasa
ambao kwa kiasi kikubwa unanufaisha zaidi mawakala badala ya wakulima moja kwa
moja.
4. RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA.
Kamati Kuu imepitisha ratiba ya
shughuli mbalimbali za Chama kwa mwaka 2015.
Aidha ratiba ya mchakato wa kuwapata
wagombea wa CCM ndani ya dola utapangwa na vikao vijavyo vya Chama.
Nape Moses Nnauye
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment