Wananchi wa kijiji cha Ijoka, Mkoani
Mbeya wameingia kwenye imani za kishirikina baada ya kuandamana na kwenda
kupasua mti ulianguka ambao wanadai una utajiri ndani yake.
Wakazi hao walisema walielezwa na
mganga wa jadi kutoka Malawi Peter Lungola, kuwa mti huo
ukitumiwa vyema utaleta utajiri.
Mganga huyo alifika kijiji humo
miaka 20 iliyopitana kuwaeleza kuw amti huo una asili kubwa ya utajiri na
kuwa chini ya mti huo kuna nyumba za kifahari zilizojaa hazina kubwa ya fedha.
Inasemekana mti huo ulianguka wiki
iliyopita na kuanza kupumua huku watu wakipata kiwewe huku nyoka mkubwa ambaye
alipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Wazee wa kijiji hicho walishangazwa
na hatua ya baadhi ya watu kula majani ya mti huo huku wengine wakichukua
magome yake na kuyahifadhi majumbani mwao.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment