
Akizungumza
na mwananchi nyumbani kwake katika mamlaka ya mji wa Rulenge mbunge huyo
amesema kuwa hahitaji kuendelea kuwa mbunge kwani umri wake nni wa kupumzika
wananchi waridhike na yale aliyoweza kwa kipindi chake.
Amesema
wakati akiingia madarakani kuongoza jimbo hilo aliahidi wananchi wa Ngara
kupata nishati ya umeme hadi vijijini na juhudi zinaendelea baada ya umeme huo
kuwashwa kupitia mpango wa usambazaji umeme vijijini (REA).
Amedai
katika tarafa ya kanazi, Nyamiaga, Murusagamba na Rulenge baadhi ya
vijiji vimepata huduma ya maji kupitia mpango wa benki ya dunia na wananchi
wamepinguza umbali wa kutafuta huduma hiyo umbali mrefu.
“Ofisi za
serikali na mashirika nimewasumbua sana wakiwemo mawaziri kuwaomba wasaidie
jimbo langu kuliwekea miundombinu ili wananchi wapambane kupunguza umaskini”.
Alisema Ntukamazina.
Alisema
changamoto kubwa katika jimbo hilo ni hisia za ubaguzi wa kijiografia
kuliingiza katika siasa kati ya jamii ya wahangaza na washubi walioko
katika kanda za Bugufi ngara kaskazini na Bushubi jimbo la Ngara kusini.
Alisema
utofauti huo unachangia wananchi kutokuwa naumoja wa dhati katika kuleta
maendeleo na kusababisha kukosa mtu makini wa kuweza kugombea nafasi ya ubunge
kwa mwaka 2015.
Katika
hatua nyingine amewaomba wananchi kupitia vikundi mbalimbali vya kijamii
kumpata mrithi wake atakaye endeleza harakati za maendeleo na asiyetengeneza
makundi ya kisiasa kidini ama kikabila wala kwa kuangalia rika.
Ntukamazina
kabla ya kuwa mbunge alikuwa katibu mkuu utumishi kati ya mwaka 1991-1993 na amewahi
kuwa msimamizi wa uboreshaji utendaji kazi na kustaafu akiwa na umri wa
miaka 55 ya kuzaliwa.
Awali
katika utumishi wake akiwa na fani ya ualimu amewahi kuwa Makamu
mkuu wa chuo cha Uongozi na maendeleo (IDM) Mzumbe 1978-1980.
Mwaka huo
aliteuliwa na Rais Mwinyi kuwa mkurugenzi wizara ya mipango na wizara ya
viwanda na biashara 1980 -1986 kabla ya kuwa katibu mtendaji wa mashirika
ya umma 425 na kuteuliwa kuwa katibu mkuu utumishi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment