![]() |
| Kamanda Wambura |
![]() |
| Joni Simon akiwa chini ya ulinzi wa polisi. |
![]() |
Polisi wakionyesha fedha bandia alizokamatwa nazo bwana Joni Simon.
|
Mashuhuda wamesema kuwa kijana huyo alinaswa katika duka moja la Tigo Pesa lililopo maeneo ya Kona Bar karibu na Hoteli ya kisasa ya Atriums.Baada ya kuwekewa pesa katika simu yake, alitoa ‘mkwanja huo bandia’ na kumkabidhi jamaa wa Tigo Pesa, lakini alizitilia mashaka fedha hizo na kulazimika kumzuia asiondoke kwanza, lakini jamaa huyo akataka kutimua mbio.
Kabla
hajafanya hivyo, jamaa wa Tigo Pesa alimrukia na kumshika huku akipiga
kelele za kuomba msaada ndipo akaupata kutoka kwa wauza chips walio
karibu.Ndipo simu ilipopigwa kwa polisi wa kituo cha Mabatini
Kijitonyama ambao wakiongozwa na Kamanda Rashidi wakaingia eneo la tukio
mara moja lakini walilazimika kutumia bunduki kumtisha ili kumtuliza
kijana huyo na kumtia mbaroni.
Baada ya
kumpekua walimkuta na kiasi cha zaidi ya shilingi laki mbili, zote
zikiwa bandia na waliondoka naye kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi
kabla ya hatua nyingine za kisheria kufuata.
Na Mwanaharakati.



No comments:
Post a Comment