Halmashauri ya wilaya ya Muleba
mkoani kagera itamekiwa kuhakikisha inasimamia mpango wa utekelezaji wa
TASAF awamu ya tatu wilayani humo ambao umezinduliwa ili kuzinusuru kaya
maskini kiuchumi.
Mkurugenzi wa TASAF ngazi ya taifa
Alphonce Kyariga amesema hayo leo wakati akifafanua malengo ya
mpango huo wilayani Muleba ambao utajumuisha
halmashauri za wilaya 53 na Muleba ikiwa ni mojawapo katika mpango
huo.
Kyariga amesema TASAF awamu ya
tatu itatekelezwa kwa kwa miaka mitatu ijayo wilayani Muleba na
kufikia kaya 17,000 kwa kuzipatia ruzuku ya fedha wakilengwa watoto
chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito.
Akizindua mpango huo mkuu wa wilaya
ya Muleba Bw Lambris Kipuyo amesema viongozi washirikiane
kuhakikisha mpango huo unakuwa mkombozi kwa jamii bila kuangalia
tofauti za kisiasa ama jografia ya vijiji na mitaa.
Kipuyo amesema taratibu za
utekelezaji wa mpango ni pamoja na umakini wa wawezeshaji katika kufanya kazi
kwa uaminifu na kuzingatia maadili na miiko ya utumishi na familia maskini
zihakikiwe na wenyeviti wa vitongoji katika vijiji.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya
ya Muleba Joseph Mkude amesema wataalamu 52 wa halmashauri hiyo
wataanza na kaya 117 katika vijijiji na mitaa kubaini
umaskini katika huduma za Afya elimu na maji na kufanya tathmini
Na Shaban Ndyamkama/ Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment