MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 31 January 2015

SOMA TAARIFA YA KUPOTEA KWA DC KIPUYO AKIELEKEA KISIWANI GOZIBA WILAYANI MULEBA

Taarifa tuliyopokea inasema  kuwa mkuu wa wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo aliondoka jana asubuhi na timu yake ya ukaguzi kuelekea kisiwani Goziba kwaajili ya kujionea hali ya wananchi na mazingira kutokana na dhoruba iliyowakumba.

Safari ya kutoka Muleba hadi Goziba ni kwa muda wa saa 6 tu, lakini wenyeji walishangaa kuona hawafiki walau saa 5 za asubuhi kwasababu walikuwa Boat yenye kasi kubwa, ikabidi waaanze kufuatilia taarifa zao,

Walifanya mawasiliano wilayani wakasema mkuu huyo wa wilaya ameondoka asubuhi lakini wakadai kuwa hawana taarifa nyingine kama amerudi bila kufika kisiwani humo, ndipo uongozi wa kisiwa ukaanza kuwatafuta ziwani, na kufanikiwa kuwapata wakiwa wamekwama ndani ya ziwa Victoria.

Kilichofuatia ni kuwavuta kutumia mtumbwi mwingine baada ya kukuta wameharibikiwa na waliokuwa nao, ambapo walifanikiwa kufika kisiwani Goziba saa 4 usiku wa kuamkia leo.

Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi, lakini mpaka sasa wakaazi ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo kisiwani humo wanaishi kwenye jengo la zahanati na wengine kadhaa wamelazwa hospitali ya mkoa Kagera baada ya kujeruhiwa na mabati yalioezuka juzi alhamisi.
Na Mwanaharakati.

No comments: