Ni kutokana na baadhi ya wamiliki wa viwanda mkoani humo
kukiuka sheria za usalama mahali pa kazi kwa kuwafanyisha kazi kinyume na
taratibu.
Hali hiyo ya kuhofia kukamatwa imekuwa ikiwafanya kufunga
Geit za viwanda vyao ili wakaguzi wa serikali wasiwafikie kama inavyoonekana
katika kiwanda cha BLANKETS & TEKTILE cha Mkuranga, huku Tanzania Gyp sum waliofungua
wamebainika kuwanyanyasa wafanyakazi kwa kuwanyima vitendea kazi huku
wakifanyika katika eneo lenye hali mbaya ya hewa.
Kiwanda hicho kinajihusisha na utengenezaji wa GYPSUM ambazo
hutumika kwenye ujenzi ambapo utengenezaji wake unahitaji vifaa kama boots,
groves na vifaa vya kuvaa usoni, lakini wao wanakiuka kama picha moja
inavyoonesha mfanyakazi akiendelea kuteseka kazini hapo juu, huku weneyewe
wachina wakijifungia kwenye vibanda vidogo vya vioo wanavyotengeneza na kuwekea
vioyozi ili waendelee kusimamia utendaji kazi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment