MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 30 January 2015

TPA KEMONDO YATAJWA KWA UNYANYASAJI WA ABIRIA WA VISIWANI, WAANDISHI WASHUUDIA KAGERA








Inatokana na kero ya kutozwa sh 600 kwenye eneo la kupandia Boat ziendazo visiwani, kwa kila anayepanda na kushuka, jambo ambalo kwao wameona ni kero ilhali eneo lenyewe ni bovu na kuwafanya wakati mwingine kudonoka kwenye maji kama unavyoona kwenye picha.

Wanasema kuwa wakihoji wanaambiwa hizo ni kwa ajili ya matengenezo ya eneo, jambo ambalo linawashangaza kwani hadi sasa hakuna matengenezo yoyote, huku wakisema kuwa mia sita kwa kupanda na kushuka ni kiasi kikubwa hata kama ni matengenezo haifai, huku wakiomba SUMATRA kuingilia kati.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: