Kwa mujibu wa Mwandishi wa Mtandao
huu kutoka Makao Makuu ya Wizaya ya Nisharti na Madini iliyoko posta jijini Dar
es Salaam ambapo ndio kuna mkutano na waandishi wa Habari uliohitishwa mahususi
kuzungumzia Hatima yake. anasema Profesa Huyo msomi wa masuala ya Miamba nchini
Ameamua Kuachia ngazi nafasi yake akidai anawaachia wengine kwenye Nafasi hiyo
kutokana na watu waameacha kuzungumzia masuala ya maendeleo wanazungumzia
mambo ya Escrow huku yeye hahusiki.
Profesa Muhongo aliongeza kuwa
hata mkataba wa Escrow ambao ndio umeleta yote hayo anasema yeye hakuwepo
wakati mkataba huo unasahiniwa.
“Mimi nashangaa leo watu kila kona
naona mimi ni mwizi, yaani kama mimi ndio nimechukua mabilioni ya escrow wakati
ukweli hupo wazi wakati wizara ya nisharti inaingia mwenye mkataba huo mimi
sikuwepo kwenye nafasi ya uwaziri,lakini leo watu bado wananiona mimi ni mwizi”
“Acha niaachia ngazi nafasi hii ya
uwaziri kwani imekuwa ni shida sana, mimi ni mtu msomi nimepata tuzo
sehemu mbalimbali duniani nasifika kwa kutoa ushahuri wenye tija,lakini leo
naonekana mwizi,wakati kiihistoria yangu mimi ni mtu msafi sina doa na wala
sijawai hata kumwibia mtu,lakini watu wananiona mimi mwizi”alisema Profesa
Muhongo.
Aidha,Profesa Muhongo alisema kabla
hajafikia hatua ya kutangaza kujiuzulu aliwasiliana na Rais Jakaya
Kikwete alimuleze hatua nayotaka kuchukua ya kujiuzulu na Rais akakubali
kujiuzulu kwake.
Vilevile Profesa Muhongo aliendelea
kukanusha kile kilichotajwa na Ripoti ya PAC iliyomtuhumu kwamba yeye alikuwa
Dalali kati ya anayejiita na kuitwa mmiliki wa IPTL ambayo sasa ni PAP Bwana
Seith na Mkurugenzi wa VIP Engineering Bwana James Rugimalira na kusema
Kamati hiyo imemuonea.
Kujiuzulu huku kwa Profesa Muhongo
kunatokana na mashinikizo mbalimbali kutoka ndani ya nchi hususani Bunge pamoja
na nchi wahisani ambao waligoma kutoa fedha za Bajeti wakitaka wakiohusika na
ufisadi wa Bilioni 320 kwenye Akaunti ya Tegeta escrow iliyokuwa benki kuu BOT
wachukuliwe hatua.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment