MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 24 January 2015

RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI NA KUWAHAPISHA, CHARLES MWIJAGE WA MULEBA NA ANNE KILANGO WAINGIZWA

Rais wa jamuhuri ya muungano Tanzania Dk Jakaya Kikwete, amewahapisha mawaziri kadhaa baada ya kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri.

Katika mabadiliko hayo, rais amewapandisha na kuwa mawaziri kamili, mh Jenista Muhagama ambaye amekuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge, naGeorge Simbachaweni ambaye amekuwa waziri wa nishati na madini.

Harison Mwakyembe amepelekwa wizara ya ushirikiano wa Afrika mashariki, na waziri wa uchukuzi amekuwa Samweli Sitta, huku Wiliam Lukuvi akiwa waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makaazi akichukua nafasi ya profesa Anna Tibaijuka.

Wengine ni Christofa Chiza aliyeteuliwa kuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji, Ummy Mwalimu naibu waziri wa katiba na sheria, Steven Masele amekuwa naibu waziri ofisi ya makamu wa rais, na Angera Kairuki ameteuliwa kuwa naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makaazi.

Charles Mwijage ameteuliwa kuwa naibu waziri wa nishati na madini, huku Bi Anne Kilango Malechela amekuwa naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi na Merry Nagu ameteuliwa kuwa naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge.

Mabadiliko hayo ya baraza la mawaziri, yamefanyika baada ya kuondolewa kwa mawaziri wa wawili wa nishati na madini na ardhi nyumba na makaazi, kutokana na sakata la fedha za ESCROW.
Na Mwanaharakati.

No comments: