MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa
Mulongo leo ameutaka uongozi wa Jiji la Mwanza kupitia kwa mkurugenzi wake
kuwapatia maeneo ya biashara wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la
Machinga wote waliopo jijijini humo.
| RC Magesa Mulongo |
Mulongo amesema wafanyabiashara hao
wapewe maeneo yao ya kufanyia biashara ili kuepusha msongamano na kurundikana
maeneo mbalimbali ya jiji hilo bila sababu za msingi wakati uwezekano wa
viongozi wa serikali kuwapa maeneo ya kufanyia kazi upo.
Mulongo ameyasema hayo leo wakati
akizungumza na Wamachinga maeneo ya soko kuu jijini Mwanza . Aidha Mhe. Mulongo
amekemea tabia ya viongozi wa serikali kuwaamuru askari wa jiji kuwapiga,
kuwakamata na kuwanyang'anya mali zao wafanyabiashara hao huku wakiwa
wameshindwa kuwapa maeneo ya kufanyia biashara.
Katika hatua nyingine, Mulongo
ameeleza kuwa amepokea maombi yote ya wafanyabiashara hao na Jumatano ijayo
watakutana katika Uwanja wa CCM Kirumba ili kufanya uchaguzi wa viongozi wao
sambamba na kukabidhiwa maeneo yao maalum kwa ajili ya kufanyia biashara.
Mulongo ameongeza kuwa ni wajibu wa
viongozi wa maeneo husika kujua majukumu yao ya kuwatumikia wananchi ili
wasilalamike kuhusu utendaji kazi wa serikali na matokeo yake kuichafua
serikali tawala ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment