MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 12 February 2015

AGIZO LA RAIS LATAJWA KUKIUKWA MANISPAA YA BUKOBA

Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi.
Wakaazi wa Kata Nyanga manispaa ya Bukoba, wameendelea kulalamikia  huduma ya umeme waliounganishwa kwa mpango wa REA, kutokana na kutofikishwa kila mtaa wa kata hiyo kama walivyofikikilia.

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema kuwa umeme umefika na wanashukuru mbunge wa Bukoba mjini aliyemwomba rais wapatiwe huduma hiyo mwaka 2013, na mwanzoni mwa mwaka huu wamepatiwa huduma hiyo ambayo hatahivyo imeishia kwenye taasisi kama kanisa, kisima cha maji, shule na zahanati pekee, huku neema hiyo ikiwasaidia wananchi walio kari bu na maeneo hayo.

Wamesema agizo la rais katika mkutano wake wa adhara, nikuwa kata nzima ipate huduma hiyo, huku wakilalamikia huduma ya maji nayo kukwama kwasababu ya umeme.

Mwenyekiti wa mtaa Iyoro akifungua kuangaliakama kuna huduma ya maji.

Mratibu wa huduma hiyo ya umeme wa kata Nyanga, amesema kuwa mpango walioelezwa na TANESCO mkoa, ni kuwa huduma hiyo imeunganishwa kwa mara ya kwanza katika taasisi, na awamu ya pili itaunganishwa   katika huduma ya pili kwa wananchi ambayo hatahivyo amesema kuwa hajui ni lini watarejea kuunganisha huduma hiyo.

Kuhusu suala la maji, wamesema kuwa utaratibu unaotumika ni kupitia umeme wa LUKU ambayo baada ya kuisha kwa mara ya kwanza wameshauriwa wajaze fomu ili waweze kulipia na baada ya hapo umeme utarejea kwenye mashine ya kusuma maji hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.

Na Mwanaharakati.

No comments: