Taarifa zinasema kuwa, mji mdogo wa Ilula, ulioko
katika mkoa wa Iringa, umekumbwa na sintofahamu kubwa kufuatia mapigano baina
ya Askari Polisi na raia.
Barabara zimefungwa na kusababisha usumbufu
mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo, huku ikielezwa kuwa gari la askari aina
ya Hyundai, limechomwa moto na raia hao, ikisemwa kuwa polisi wamezidiwa.....
Inaelezwa kuwa, asubuhi ya leo, askari walifika
katika eneo hilo kwa minajili ya kukamata watu waliokuwa katika vilabu wakinywa
pombe muda huo wa kazi, ambapo katika kimbia kimbia ya wananchi kuwaepuka
askari hao, mama mmoja alianguka ghafla na kupoteza maisha.
Chanzo chetu kinaendelea kutanabaisha kuwa, mama
huyo alikuwa hajaguswa na askari hao, lakini wananchi ghafla wakaanzisha fujo
wakidai kuwa kifo cha mama huyo kimetokana na askari hao na ndipo tafrani baina
ya pande hizo mbili likazuka.
Hadi taarifa hizi zinawekwa hewani, inaelezwa
kuwa askari walishazidiwa na kuwa walishaomba msaada wa Askari wa Kikosi cha
Kuzuia Fujo (FFU), toka Iringa mjini, ambao walikuwa njiani kuelekea eneo la
tukio.
Taarifa zaidi kuhusu tukio hili zitawajieni,
pindi mawasiliano na mamlaka yatakapokamilika
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment