 |
| Mwenyekiti wa mkutano wa sherehe maadhimisho ya siku ya redio duniani
ambaye pia ni Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw.
Allan Lawa akiendesha mada chokonozi kuwa ni kwa namna gani radio
inaweza kutumika kama jukwaa la ushiriki kwa vijana katika mabadiliko ya
kidemokrasia? Utafiti unaogusa Watanzania wakielekea katika uchaguzi
mkuu.
Na Mwandishi wetu, Arusha
Vyombo vya habari hususan redio za jamii zimetakiwa kutanguliza
uzalendo na kutetea maslahi ya taifa ili kuliepusha taifa katika
migogoro na mitafaruku inayoweza kusababisha machafuko nchini hasa
katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
Nyerembe Munasa wakati wa kuadhimisha Siku ya Redio duniani iliyofanyika siku chache zilizopita.
Akizungumza na watangazaji wa redio za jamii na wadau mbalimbali wa
habari nchini katika ufunguzi wa maadhimisho hayo Munasa alisema redio
ina nguvu kubwa kuchambua na kutengeneza mustakabali wa taifa na hasa
vijana iwapo itatumika vizuri badala ya kuwa chanzo cha matatizo na
uchochezi mambo ambayo yanaweza kulisambaratisha taifa.
Amewataka waandishi na watangazaji wa redio jamii kuzingatia maadili
ya kazi zao kwa lengo la kuleta mabadiliko katika maisha ya Watanzania
na kujenga taifa endelevu .
|
 |
| Mkongwe na mkufunzi wa tasinia ya habari kutoka chuo kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), Ayub Rioba akitoa mada Je uwekaji huru wa mawimbi ya
radio kumesababisha mambo mabaya zaidi kuliko mazuri: Mitazamo na
matarajio kuhusiana na ushiriki wa vijana wakati wa sherehe za
maadhimisho ya siku ya redio duniani. |
 |
| Meneja wa Kituo cha redio ya Jamii FADECO, Adeline Lweramula akitoa neno
la shukrani kwa shirika la UNESCO kwa kuwawezesha kukutana na
kubadilishana mawazo kwenye maadhimisho hayo. |
 |
| Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, Nyerembe Munasa (wa pili kulia)
akiagana na baadhi ya wadau wakongwe katika tasnia ya habari mara baada
ya kuhitimisha maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Arusha. |
Sherehe hizo ambazo huandaliwa kila mwaka tarehe 13 Februari,
ziliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) na ujumbe wa mwaka huu ni “Nguvu ya Redio na Ushiriki
wa Vijana katika Maendeleo”.
Ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova katika
kuadhimisha siku hiyo na kusomwa kwa niaba yake na mwakilishi wa UNESCO
nchini Bokosha Spencer umesisitiza nguvu ya radio katika kujihusisha na
masuala ya kijamii kwa vijana wenye umri chini ya miaka 30, ambao ni
zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani .
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment