Kiungo wa timu ya
Coastal Union, John Mahundi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Disemba
2014 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja
mbalimbali nchini.
Mahundi alitoa mchango
mkubwa kwa timu yake ya Coastal Union mwezi Disemba mwaka jana na kuchaguliwa
na jopo la makocha linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora wa kila mwezi.
Aidha mshambuliaji wa
timu ya..............
Polisi Morogoro, Said Bahanuzi amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi
Januari 2015 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi mzunguko
wa 15 kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Bahanuzi anayechezea
timu ya Polisi Morogoro kwa mkopo akitokea timu ya Young Africans amekua na
mchango mkubwa kwa timu yake tangu kujiunga nayo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu
ya Vodacom nchini.
Kwa kuibuka wachezaji
bora, Mahundi na Bahanuzi watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila
mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo maalumu la makocha
waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa
kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata
mshindi wa mwezi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment