MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 17 February 2015

MH. EDWARD LOWASA APEWA MSAADA JIMBONI

Mmiliki wa kiwanda kikubwa cha A to Z cha Arusha,Anoji Shah (aliesimama) akiwaeleza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli umuhimu wa elimu na pia kutangaza msaada wa enzi wa mabweni yote mawili yaliyoteketezwa kwa moto wiki mbili zilizopita.
 Ni katika kumuunga mkono katika kupounguza changamoto za kielimu jimboni kwake.
Lowassa ambaye alirejelea kauli yake ya kwamba yeye si tajiri bali ni tajiri wa marafiki, alichangia shilingi milioni tatu kwa ajili ya sare za shule kwa wanafunzi ambao nguo zao ziliteketea.Aidha mwenyekiti mtendaji wa makampuni IPP amechangia shilingi milioni 25 kwa ajili ya vitanda.


Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli wakati alipoitembelea leo.


Na Mwanaharakati.

No comments: